Joy FM

Mkandarasi apewa siku 3 kukamilisha barabara

26 June 2024, 12:51

Mkuu wa wilaya Kigoma akikagua barabara ya Kalinzi hadi Mkabogo, Picha na Sadik Kibwana

Barabara ya Kalinzi – Mkabogo katika halmashauri ya wilaya Kigoma imekuwa haipitiki kwa muda mrefu kutokana na mvua zilizonyesha na kusababisha mkandarasi kufanya ujenzi katika barabara hiyo inayotegemewa na wakati wa kata hiyo kwa shughuli za usafirishaji wa bidhaa

Na Sadik Kibwana – Kigoma Dc

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli ametoa muda wa siku tatu  kuanzia leo mpaka ijumaa Kwa mkandarasi MBUYA’S Contractor anayetengeneza barabara ya Kalinzi – Mkagobo  kuhakikisha ameikamilisha barabara hiyo.

Mhe Kali ametoa maagizo hayo baada ya Kufika na kujionea hali ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 6 na kutoridhishwa na utendaji KAZI wa mkandarasi huyo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya kigoma alum kalli

Kwa upande wake  kaimu wa Mradi tarura mkoa mhandisi John Rumbiza amesema mkandarasi aliwepa KAZI hiyo toka mwaka jana alipaswa kuikamilisha barabara hiyo mwezi machi mwaka huu.

Sauti ya kaimu msimamizi wa mradi kutoka TARURA

Naye mwenyekiti wa CCM kata ya Kalinzi Abdallah Kilumbi Lutti akizungumza Kwa niaba ya wananchi amefurahishwa na ujio wa mkuu huyo wa wilaya na kusema kuwa kukwama kwa barabara hiyo Imefanya washindwe kusafirisha mizigo Yao Kwa Wakati kitu ambacho kinafanya wabaki kuwa masikini.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM kata ya kalinzi