Watoto elfu 60 hawapati chakula shuleni
18 June 2024, 16:27
Wazazi na walezi wilayani kasulu mkoani kigoma wametakiwa kuendelea kuunga mkoano juhudi za serikali katika kuchangia chakula shuleni ili kusaidia kudhibiti utamlo kwa watoto wa shule za msingi na sekondari.
Na Michael Mpunije – Kasulu
Zaidi ya watoto elfu 60 wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma hawapati huduma ya chakula shuleni kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kuchangia chakula kwa watoto wao.
Akizungumza na wazazi na pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari katika tarafa ya makere halmashauri ya wilaya ya Kasulu Afisa lishe katika halmashauri hiyo Bw. Kingolo sayi amesema halmashauri hiyo ina zaidi ya watoto laki 1 wa shule za msingi na sekondari kati ya hao ni watoto elfu 40 pekee wanaopatiwa huduma chakula shuleni.
Amesema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mpango wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote wa shule za msingi na sekondari wanapata huduma ya chakula shuleni ili kukabiliana na lishe duni kwa watoto.
Aidha bw. Kingolo ameongeza kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa kuona umuhimu wa kuchangia chakula shuleni kutokana na kipato kuwa kidogo na kuwasisitiza kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na utapiamlo kwa watoto.
Baadhi ya wazazi katika kata ya makere wameiomba serikali kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi katika kuhamasisha kuchangia chakula shuleni ili kukakabiliana na suala la utoro