Joy FM

Wananchi Kigoma waonywa kufanya shughuli hifadhi ya barabara

14 June 2024, 12:27

Wananchi wametakiwa kutofanya shughuli za kibindamu karibu na hifadhi za barabar, Picha na Mtandao

Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imewataka wananchi kuacha kuharibu barabara kupitia shughuli za binadamu ikiwemo kilimo na ukataji miti na kutupa taka barabarani.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wananchi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya kutumia eneo la barabara kwa kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo ufyatuaji wa tofari jambo linalopelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilayani Kasulu mkoani Kigoma Mhandisi Eric Raban wakati akizungumza na madiwani wa halamshauri ya Mji Kasulu katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa halmashuri hiyo.

Mhandisi Raban amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kufanyia shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya barabara kitu ambacho ni kosa kisheria.

Sauti ya Kaimu meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilayani Kasulu mkoani Kigoma Mhandisi Eric Raban

Aidha Mhandisi Raban hapa anatolea ufanyanuzi wa adhabu atakayoipata mwananchi atakaye tumia eneo la hifadhi ya barabara pasipo kupata kibali cha serikali.

Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu wamesema ni vizuri elimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi waishio mijini na vijijini ili kuwaepusha na faini hiyo maana wengi wanafanya hivyo pasipo kujua sheria hiyo.

Sauti ya wananchi wilayani kasulu