Joy FM

Wanachuo 48 FDC Kibondo wapatiwa msaada

14 June 2024, 12:06

Baadhi ya wanafunazi wa FDC Kibondo wanaosoma kozi mbalimbali ikwemo ufundi, Picha na Mtandao

Shirika la Social Action Trust Fund (SATF) limetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni mkakati wa kusaidia kuendeleza ujuzi kwa wananfunzi wanaoupata chuoni hapo FDC Kibondo.

Na James Jovin – Kibondo

Wanafunzi wa fani ya ufundi stadi wapatao 48 waliohitimu mafunzo katika chuo cha FDC Kibondo wamepatiwa msaada wa vifaa vya ufundi stadi kupitia mradi wa kuhudumia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu unaofadhiliwa na shirika la Social Action Trust Fundi (SATF) ikiwa ni mkakati wa kuwapa maarifa na ujuzi utakaowasaidia kufikia ndoto zao katika Maisha.

Vifaa vilivyotolewa kwa wanafunzi hao ni pamoja na cherehani, vifaa vya ufundi wa bomba, ufundi wa umeme, vifaa vya ufundi wa magari ikiwa ni sambamba na vifaa vya kufundishia elimu ya awali kwa wale waliosomea fani hiyo.

Baadhi ya wanafunzi waliopokea msaada huo wameshukuru sana shirika la Social Action Trust Fundi SATF kwa msaada huo wa vifaa vya ufundi vitakavyowasaidia kwa namna moja ama nyingine katika Maisha.

Sauti ya Baadhi ya wanafunzi waliopokea msaada huo

Kwa upande wake afisa mradi wa kuhudumia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia shirika la SATF Bw. Sengiyumva Bisaga amesema kuwa licha ya juhudi hizo za kuwakomboa vijana katika wimbi la umasikini lakini kumekuwepo na changamoto mbali mbali ikiwemo utoro wa kuhudhulia mafunzo ya ufundi yanayotokana na wengi wao kubebeshwa ujauzito kwa upande wa wasichana.

Sauti ya afisa mradi wa kuhudumia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia shirika la SATF Bw. Sengiyumva Bisaga

Naye afisa maendeleo ya jamii bw. Andrew Kapinye pamoja na afisa ustawi wa jamii wilayani Kibondo bi. Sophia Gwamagobe ambao walialikwa katika shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa vya ufundi stadi kwa wanafunzi hao wamewataka wanafunzi hao kuthamini msaada huo na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii bw. Andrew Kapinye pamoja na afisa ustawi wa jamii wilayani Kibondo bi. Sophia Gwamagobe