Joy FM

Viongozi watakiwa kuwa makini kwenye kutoa maamuzi

11 June 2024, 16:45

Waumini wa kanisa la anglikana Mt. Andrea kasulu mjini, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali kupitia viongozi wanaoteuliwa na kuaminiwa kushika nyadhifa mbalimbali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wametakiwa kusimama imara na kufikiria mara mbili kabla ya kuhukumu au kutamka kitu.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Viongozi wenye mamlaka katika serikali na idara mbalimbali wametakiwa kuwa makini katika kutoa maamuzi kutokana na kuwindwa na shetani.

Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la anglikana Tanzania Dr. Donard Mtetemela amebainisha hayo wakati akizungumza katika kilele cha kongamano la wanaume lililofanyika kwa siku tatu mfurulizo katika kanisa la Mt Andrea anglikana Kasulu Mjini dayosisi ya western Tanganyika Mkoani Kigoma.

Amesema viongozi wengi wenye dhamana ya kufanya maamuzi kwa watumishi wengine ya kuwapandisha vyeo ama kuwaidhinishia stahiki zao mikono yao inawindwa na shetani ili kuitumia vibaya.

Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la anglikana Tanzania Dr. Donard Mtetemela akiwa na askofu Bwata

Aidha Askofu Dr. Mtetemela amesema viongozi wanapaswa kuhakikisha wanamcha Mungu ili kuepuka kufanya vitendo vya rushwa na ufisadi ambavyo vimeonekana kufanyika kutokana na mikono yao kutumika vibaya na shetani.

Sauti ya Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la anglikana Tanzania Dr. Donard Mtetemela

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Emmanuel Bwatta aliyeandaa kongamano hilo amesema lengo la kufanya kongamano hilo ni kuwakumbusha wababa wajibu wao katika kanisa na jamii kwa ujumla.

Sauti ya Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la anglikana Tanzania Dr. Donard Mtetemela

Nao baadhi ya wanaume walioshiriki katika kongamano hilo akiwemo mwinjilisti Osman Bonabucha Hwago, Mchungaji Shadrack Nyemera na Filmon Daud wamesema kongamano hilo limewasaidia kwa kiasi kikubwa kujua wajibu wao wa kulihudumia kanisa, familia na jamii kwa ujumla.

Sauti ya wanaume walioshiriki katika kongamano