Wananchi watakiwa kuzingatia usafi wa mazingira
5 June 2024, 13:32
Serikali wilayani kasulu mkoani kigoma imesema haitawafumbia wananchi na taaisisi ambazo hazizingatii usafi wa mazingira ili kuhakikisha magonjwa ya mlipuko yanadhibitiwa.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wananchi wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Wametakiwa desturi ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya Mlipukoikiwemo kipindu pindu.
Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani Mjini Kasulu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuzingatia usafi wa mazingira kila wakati na kuacha imani potofu kuwa suala la usafi linafanyika msimu wa mvua pekee.
Amesema viongozi wa halmashauri na wilaya wamefanya usafi maeneo mbalimbali wilayani humo ili kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa kufanya usafi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye licha ya kumshukuru Mkuu wa wilaya ya Kasulu kwa namna alivyokuwa mfano katika zoezi hilo, amesema zoezi la usafi linafanyika kila siku ya jumatano ili kuhakikisha maeneo ya huduma za jamii ikiwemo sokoni yanakuwa safi na salama.
Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu akiwemo Julius Lameck, Asifiwe Zaledi na George Mamboleo wamesema usafi wa mazingira ni wamuhimu sana ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.