Joy FM

“Wanawake wanabakwa na hawatoi taarifa Kasulu”

5 June 2024, 12:55

Ni katika mkutano wa kuhamasisha na utoaji wa elimu ya ukatili wa wilayani kasulu, Picha na Mtandao

Vitendo vya ubakaji kwa wanawake hasa wanaojishughulisha na kilimo katika maeneo ya mashambani wilayani kasulu vimeendelea kushamiri huku wahanga wakiogopo kutoa taarifa za vitendo hivyo kwa kuhofia kuacha na wenza wao.

Na Michael Mpunije

Wananchi wilayani Kasulu mkoani kigoma wameiomba serikali kuimarisha ulinzi dhidi ya wanawake ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa maeneo ya shambani.

Wananchi hao akiwemo Agripina mlobezi na Auzebiusi kimondo wamesema matukio hayo yametajwa kutokea hasa eneo la kigule ambapo hufanyika shughuli za kilimo.

Wamesema ikiwa ulinzi utaimarishwa utasaidia wanawake kufanya shughuli za kilimo kwa uhuru.

Sauti za wanawake wakieleza madhira wanayokutana nayo wakiwa shambani wengi wakibakwa

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji kasulu Bi,Tausi baracka amesema wanafuatilia taarifa hizo licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto hiyo miaka iliyopita wakati afisa mtendaji kata ya mrusi Omari sebabili akiwataka wanawake kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.

Sauti ya afisa ustawi wilaya Kasulu na afisa mtendaji wa kata

Mkuu wa wilaya ya kasulu kanali Isaac mwakisu amesema wanaendelea kuhakikisha usalama unaimalika katika wilaya nzima ya kasulu baada ya kubainika uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu

Hata hivyo wananchi wameshauriwa kushirkiaana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.