Joy FM

Kasulu yasisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia

29 May 2024, 12:05

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu mwalimu Vumilia Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Jamii katika halmashauri ya mji wa kasulu mkoani kigoma imetakiwa kuzingatia matumizi ya nishati safi ya kupikia kama sehemu ya mpango mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma imesema imejipanga kutekeleza maagizo ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuielimisha jamii juu ya namna bora ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuepuka matumizi ya kuni na mkaa yanayopelekea madhara kwa mtumiaji na  uchafuzi wa mazingira.

Haya yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye wakati akizungumza na radio joy fm ofisini kwake ambapo amesema kampeni hiyo ya serikali itatekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu katika halmashauri hiyo ili kuisaidia jamii kuondokana na changamoto inayopitia kwasasa.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kasulu vumilia simbeye

Aidha Mwl. Simbeye ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyotekeleza wajibu wake wa kumletea maendeleo mwananchi wa halmashauri ya Mji Kasulu na mkoa wa kigoma kwa ujumla.

Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu

Kwa upande wake Judith Bashigwa ni mkazi wa halmashauri ya Mji Kasulu yeye anayetumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia anasema utumiaji wa kuni na mkaa unaharibu mazingira sambamba na kuleta madhara mwakubwa kwa mtumiaji tofauti na mtumiaji wa nishari safi ya gesi.

Pia amesema anatumia kuna na mkaa kwasababu ya gharama za matumizi ya gesi kuwa juu ukilinganisha na matumizi ya kuni na mkaa.

Sauti ya wananchi mjini kasulu

Huku Asha Kibacha ambaye ni mama anayetumia nishati safi ya gesi anazungumzia namna ilivyo rahisi na faida kwa mtumiaji wa nishati safi ya gesi tofauti na matumizi ya kuni na mkaa.

Sauti ya watumiaji ya nishati safi ya kupikia