TASAF yageuka neema kwa kaya masikini
28 May 2024, 10:31
Serikali wilayani kibondo mkoani kigoma imesema mpango wa kunusuru kaya masikini umesaidia kaya nyingi kujinusuru na umasikini kupitia elimu ya namna ya kutumia fedha wanazopewa katika kuzalisha mali ikwemo ufugaji.
Na James Jovin – Kibondo
Baadhi ya kaya masikini katika kijiji cha Kumkugwa wilayani kibondo mkoani kigoma wamesema kuwa wamenufaika na mradi wa TASAF kiasi cha kuweza kujenga nyumba za bati, kusomesha watoto shule na kufuga mifugo
Wamebainisha hayo wakizungumza na radio Joy wakati wakipewa mafunzo ya namna bora ya kujikwamua na lindi la umasikini ili mradi huo wa TASAF utakapoisha waweze kuendelea na maisha kama kawaida
Bi. Elizabeth Kabika pamoja na bi. Godberter Fransisco ni miongoni mwa wanufaika wa tasafu katia kijiji cha Kumkugwa wilayani Kibondo na hapa wanaelezea jinsi walivyonufaika na kujikwamua katika lindi la umasikini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Kumkugwa bw. Damian Gwimo ameitaka serikali kuendelea kuwajali wananchi hasa wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwakwamua katika lindi la umasikini na kuleta maendeleo endelevu miongoni mwa jamii.
Nae mratibu wa TASAF wilayani Kibondo bw. Dotto Makunja amesema kuwa katika wilaya ya Kibondo zaidi ya kaya elfu kumi zimenufaika na mradi wa kunusuru kaya masini TASAF ambapo wameweza kujikwamua katika matatizo mbali mbali na kukidhi mahitaji ya msingi katika maisha ya kila siku.