DC Kigoma ahimiza waumini kujiandikisha daftari la mpiga kura
27 May 2024, 14:36
Wakati zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura likitarajiwa kuzunduliwa julai mosi mwaka mkoani kigoma, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wametakiwa kuhimizi waumini na jamii kwa ujumla kujitokeza kujiandikisha kwenye zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.
Na Prisca Kizeba – Kigoma
Mkuu wa Wilaya Kigoma Mh. Salum Kalli amewataka viongozi wa dini ya kikristo Mkoani Kigoma kuwahiza waumini wao kujitokeza kujiandikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ambalo linatarajiwa kuznduliwa mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu mkoani hapa.
Mh. Kalli amesema hayo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la (EAGT) Mwasenga ambapo amesema kuwa viongozi wa Dini ni chachu kubwa ya kuhimiza watu kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.
Aidha Mh. Mkuu wa wilaya Kigoma amesema ni lazima waumini wasimame katika imani na kuendelea kuliombea taifa ili kudumisha amani.
Kwa upande wake, Mkuregenzi msaidizi wa utafiti wa sayansi ya mistu kutoka taasisi ya Jane Goodal Dkt Zabibu Kabalika ameiomba jamii kuona umuhimu wa kutunza mazingira ili kudhibiti hali ya mabadiliko ya tabii ya nchi.
Naye mchungaji wakanisa hilo Agustino kizeba ambaye pia ni Mwenyekitiu Msaidizi wamakanisa ya Kipetekoste (CPCT) amemuahidi Mkuu wa Wilaya kuwa atawahimza waumi pamoja viongozi wote wa dini kujtikeza katika kujiandikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ambalo linatarajiwa kuzinduliwa mwezi julai.
Hata hivyo badhi ya waumini waliohudhuria ibaada hiyo wakaeleza.