Joy FM

Zaidi ya watoto elfu 10 wadumaa Kibondo

27 May 2024, 09:29

Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wilayani kibondo Mkoani Kigoma, Picha na James Jovin

Serikali wilayani kibondo mkoani kigoma imesema itaendelea kutumia siku ya afya na lishe ya kijiji kutoa elimu ya namna ya kuanda lishe bora kwa wananchi ili waweze kufahamu namna ya kukabiliana na lishe duni kwa watoto ambao wameonekana kuwa na tatizo la udumavu licha ya kuwa na vyakula vya kutosha.

Na James Jovin – Kibondo

Zaidi ya watoto elfu kumi wenye umri chini ya miaka mitano katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma walikutwa wamedumaa baada ya kupimwa hali ya lishe wakati wa maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya kijiji katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Hayo yamebainishwa na kaimu afisa lishe wa wilaya ya Kibondo bi. Juckline Sospeter akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe zilizofanyika katika kipindi cha miezi sita iliyopita

Aidha bi. Jackline amesema kuwa taarifa hiyo ya watoto zaidi ya elfu kumi waliokutwa na udumavu ilikusanywa katika vijiji hamsini vilivyofanya maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya kijiji wilayani kibondo.

Sauti ya afisa lishe wilayani kibondo mkoani Kigoma

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Dr. Gabriel Chitupila amesema katika kupunguza ama kumaliza hali hiyo ya udumavu kwa watoto ni vema viongozi wa kisiasa na kidini kushiriki kikamilifu na kuweka agenda za lishe wanapozungumza na wafuasi wao.

Sauti ya kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya kibondo

Nae mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amesema kuwa lishe ni agenda ya serikali katika kutokomeza utapiamlo, udumavu na ukondefu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano hivyo kila mtu anapaswa kushiriki katika kutokomeza tatizo hilo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kibondo mkoani Kigoma