Joy FM

TASAF yasaidia kupunguza mimba kwa mabinti

23 May 2024, 08:23

Mnufaika na mfuko wa kunusuru kaya masikini wilayani uvinz mkoani kigoma, Picha na Orida Sayon

Serikali wilayani uvinza mkoani kigoma kupitia kwa mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini Nchini TASAF imesema kuwa ruzuku zinazotolewa kwa kaya masikini zimesaidia kupungunguza umasikini ambao ulikuwa ukisababisha ukatilii hasa kwa watoto wa kike kuolewa katika umri mdogo.

Na Kadislaus Ezekiel – Uvinza

Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini nchini TASAF Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi, baada ya kuanzisha miradi ya ufugaji wa Mbuzi na Kuku, Hatua ambayo imesaidia Baadhi yao Kujikwamua Kiuchumi.

Wakizungumza na Viongozi wakati wa tathimini ya fedha zinazotolewa na Serikali Kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF Baadhi ya Wanufaika wamesema, licha ya kujikita na ufugaji baadhi yao wamefanikiwa Kukamilisha Ujenzi wa nyumba za Makazi baada ya kuweka akiba ya fedha na kuuza mifugo yao.

Sauti ya wanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini uvinza

Kwa upande wake Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya Masikini TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Dismas Marere, amesema Serikali Imetoa zaidi ya Bilioni Sita kwa kipindi cha miaka mitatu ambazo zimesaidia kuinua uchumi wa Vijana waliopo katika kaya Masikini pamoja na wazazi kwa ujumla.

Sauti ya mratibu wa tasaf wilayani uvinza Dismas Marere