Joy FM

Madiwani Kigoma Ujiji wakerwa utendaji kazi mbovu wa mkurugenzi

17 May 2024, 15:29

Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Lupoli akiwa katika Baraza la Madiwani, Picha na Josephine Kiravu

Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji yupo hatarini kupigiwa kura ya kumkataa baada ya madiwani kumtuhumu kuwa hashirikiani na viongozi wa manispaa hiyo na kuwa chanzo cha miradi ya maendeleo kushindwa kusonga mbele.

Na, Josephine Kiravu – Kigoma

Baraza la madiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji limeonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na kulazimika kuazimia kubadili baraza hilo na kuwa kamati ili kujadili masuala ya kiutumishi ambayo yanakwamisha utekelezaji wa baadhi ya miradi ikiwemo ujenzi wa wodi ya kina mama kituo cha afya Buhanda.

Hiyo ndio ilikuwa hali halisi mara baada ya katibu wa kikao cha baraza la madiwani ambaye ni MKurugenzi wa Manispaa ya kigoma ujiji kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Baraka Lupoli.

Hata hivyo Mwanasheria wa Manispaa hiyo Lessi Majala akamama na kulitaka baraza hilo la madiwani wasiridhiekauli ya mstahiki Meya iliyowataka kubadili baraza hilo la madiwani kuwa kamati ili kujadili masuala ya kiutumishi ambayo yalikuwa yakimlenga mkurugenzi.

Sauti ya mwanasheria wa manispaa ya Kigoma Ujiji

Na hapa Diwani wa Kata ya Buhanda Kilahumba Glibert akaeleza yale ambayo alijionea kwenye kata yake wakati wa ziara ya kamati ya fedha ambapo aliungana na Msatahiki Meya kubadili baraza hilo kuwa kamati kwa muda.

Sauti ya diwani wa kata ya Buhanda

Na hapa Mstahiki meya akatoa maelekezo ya baraza hilo kugeuka kuwa kamati akitumia kanuni ya 88 ambayo ilisomwa na Diwani wa kata ya machinjioni Seif Foadi.

Sauti ya meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji

Mara baada ya maelekezo hayo kamati hiyo iliketi kwa zaidi ya saa 5 ambapo wananchi, watendaji wa kata na waalikwa wengine walikuwa nje ya ukumbi wakisubiri hatma ya kamati hiyo na haya ndio majibu ya mstahiki Meya.

Sauti ya meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji