Joy FM

Vyakula kwenye chupa zilizotumika kuhatarisha afya Kasulu

9 April 2026, 17:09

Muonekano wa chupa za maji zilizokwishatumika zikiwa zimewekwa mafuta, Picha na Emmanuel Kamangu

Matumizi ya chupa zilizotumika kufungashia vyakula si salama kwa sababu yanaweza kusababisha magonjwa ya tumbo, sumu mwilini, na madhara ya muda mrefu kiafya.

Na Emmanuel Kamangu

Wanaotumia  maziwa, asali, juisi na mafuta ambayo  hutunzwa katika vifungashio vya  chupa za plasitiki zilizokwisha kutumika wako hatarini kukumbana na magonjwa mbali mbali hasa magonjwa ya tumbo.

Kumekuwa na wimbi  kubwa la wajasiliamali na baadhi ya wafanyabiashara kufunga vitu mbali mbali katika Chupa  zilizokwisha kutumika hasa chupa za  maji na soda jambo linalotajwa ni hatari kwa afya ya mlaji..

Akizungumza na Redio  Joy Fm,   Mratibu wa huduma za shirika la Viwango Tanzania TBS katika halmashauri ya mji wa kasulu  Bw. Gribeti mosh amesema chupa   za vinywaji  zilizotoka kutumiwa na  mtumiaji  zinapotumika kama vifungashio  huweza kupeleka mlaji kukumbana na athali mbali mbali za kiafya na kuomba wananchi kuepuka kununua hasa maziwa na mafuta ya kula ambayo yamefungwa katika chupa za maji na soda ambazo tayari zimekwisha kutumika.

Mratibu wa huduma za shirika la viwango Tanzania TBS Halmashauri ya mji wa KASULU Bw. Grebet Mosh, Picha na Emmanuel Kamangu

Aidha Bw. Mosh amewasihi sana wajasiliamali na wafanyabiashara kuhakikisha wanafunga bidhaa zao za chakula na vinywaji katika vifungashio vinavyoruhusiwa na shirika la viwango Tbs ili kulinda afya ya mlaji.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema mtindo wa maisha na uhaba wa elimu imekuwa ni moja ya chanzo kinachopelekea kutumia vitu vingi bila kujali usalama wa afyya zao.

Hata hivyo wananchi hao wameongeza kuwa serikali inawajibu wakuendelea kusimama kidete kuhakikisha wanaotumia makopo kufungashia bidhaa mbali mbali  wanachukuliwa hatua za kisheria.

Sauti ya Mwanahabari wetu Emmanuel Kamangu