Joy FM

Radi yaua mmoja, wawili wanusurika Kasulu

8 April 2026, 13:17

Picha na Mtandao

Radi ni tukio la kiasili linalotokea wakati wa mvua kubwa na mawingu mazito, likihusisha umeme wenye nguvu unaoshuka kutoka angani kwenda ardhini na tukio hili linaweza kuwa hatari kwa maisha ya binadamu na mali.

Na Michael Mpunije

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Maiko Samwel mkazi wa Kitongoji cha Katezi Kijiji na kata ya Kagerankanda Halmshauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya kupigwa na radi huku watu wawili wa familia moja wakisunurika kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha katika kata hiyo.

Akizungumza na Radio Joy Fm kwa njia ya Simu mwenyekiti wa Kitongoji cha Katezi Bi. Fatuma Issaya amesema tukio hilo limetokea April 6 mwaka huu wakati mwanaume huyo akiwa ameenda kuvua Samaki kwenye Moja bwawa lililopo katika kata hiyo.

Amesema baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa vipimo na daktari wamebaini kuwa mwanaume huyo alifariki kwa kupigwa na radi huku kukiwa na alama za chale sehemu za mwili wake kulingana na mwenyekiti wa kitongoji hicho.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Katezi Bi. Fatuma Issaya

Baadhi ya wakazi wa kata ya Kagerankanda wamesema mwanaume huyo ameacha mke mmoja na Watoto watatu hivyo wameiomba jamii kuendelea kushirikiana na familia ya marehemu kwa kumtia moyo hasa katika kipindi hiki.