Joy FM

Ujenzi ofisi za Halmashauri wafikia zaidi ya 90% Kibondo

8 April 2026, 13:02

Muonekano wa ofisi mpya za Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Picha na Ofisi ya Mawasiliano Kigoma

Mradi unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.9 ambapo utakapokamilika utawarahisishia wananchi  kupata huduma sambamba na kuimarisha utendaji kazi kwa watendaji kutokana na  matumizi ya jengo hilo.

Na Kadislaus Ezekiel

Wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wamepongeza serikali kwa kutenga fedha kiasi cha zaidi ya bilioni mbili, ili kujenga ofisi za kisasa za Halmashauri hiyo, ikiwa ni mkakati wa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi katika eneo moja, na kuondoa usumbufu kwa jamii kutembea umbali mrefu kusaka huduma.

Ujenzi wa mradi wa ofisi za Halmashauri hii ya Kibondo, unaendeela kufikia hatua za mwishoni, matumaini makubwa yakija kwa wananchi kurahisisha upatikanaji wa huduma katika eneo moja, na kuokoa mda wa kutafuta ofisi za idara tofauti.

Muonekano wa ofisi mpya za Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Picha na Ofisa ya mawasiliano Kigoma

Katika taarifa ya kaimu mhandisi mkuu wa idara ya miundombinu Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Edwin Edward, amesema mradi huo upo katika hatua za mwishoni, na shughuli zilizobaki zinaendelea kufanyiwa kazi kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

Sauti ya Mwandishi wetu Kadislaus Ezekiel