Joy FM
Joy FM
6 April 2026, 12:51

Jamii imeendelea kukumbushwa umuhimu wa kudumisha upendo na amani kama msingi wa maisha ya imani na mshikamano wa kijamii.
Na Hagai Ruyagila
Waumini wa dini ya Kikristo katika Kata ya Murufiti, Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma, wameaswa kuendelea kuishi katika upendo ili kujenga jamii yenye, amani, mshikamano na maadili mema.
Rai hiyo imetolewa na Mwinjilisti Titus Ndahilo wa kanisa FPCT Mkombozi wakati akihubiri Neno la Mungu katika mkutano wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste uliofanyika katika Kata ya Murufuti Mjini Kasulu.
Akizungumza katika Ibada hiyo, Ndahilo amesema kuwa upendo wa kweli umepungua miongoni mwa Wakristo waliowengi, huku akibainisha kuwa palipo na upendo wa kweli, kuna uvumilivu hata pale mtu anapokosea kwa kuwa asili ya upendo ni mungu mwenyewe.
Kwa upande wake, Mchungaji msaidizi wa Kanisa la FPCT Murufiti, Misheni ya Kasulu Mjini, Ibrahimu Katenza amesema upendo una thamani kubwa kwa Mkristo, na kusisitiza kuwa bila upendo maisha yangekuwa magumu sana.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada hiyo wamesema kuwa upendo una umuhimu mkubwa ndani ya jamii, kwani kwa kuonyesha upendo kwa wengine wanatimiza agizo la Mungu.