Joy FM

Wananchi walia na vitendo vya uhalifu Kasulu

1 April 2026, 12:40

Mkaguzi msaidizi wa Polisi Willy Lupa ambaye ni Polisi kata wa kata ya Nyamnyusi, Picha Hagai Ruyagila

Ulinzi shirikishi ni mfumo wa usalama unaohusisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola kama vile polisi katika kulinda maisha na mali za watu na mfumo huu umeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vitendo vya uhalifu katika jamii mbalimbali.

Na Hagai Ruyagila

Wananchi wa Kijiji cha Nyamnyusi, Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto ya vitendo vya uhalifu, hususan wizi vinavyotokea mara kwa mara katika maeneo yao.

Ombi hilo wamelitowa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko la Nyamnyusi, ambapo wakazi hao wameeleza kuwa matukio ya wizi yamekuwa yakiongezeka na kusababisha hofu kubwa.

Mkaguzi msaidizi wa polisi Willy Lupa ambaye ni polisi kata wa kata ya Nyamnyusi akizungumza na uongozi wa Kijiji na kata ya Nyamnyusi kuhusu ulinzi na usalama, Picha na Hagai Ruyagila

Wamesema kuwa wanahitaji hatua madhubuti zichukuliwe ili kurejesha hali ya utulivu na kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa kama ilivyokuwa hapo awali.

Sauti ya Wananchi wa Kijiji cha Nyamnyusi

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamnyusi Japhet Ntabaha amekiri kuwepo kwa vitendo vya kihalifu, ikiwemo wizi na kueleza kuwa ni changamoto inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Sauti ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamnyusi Japhet Ntabaha

Naye, Mkaguzi msaidizi wa Polisi Willy Lupa ambaye ni Polisi kata wa kata ya Nyamnyusi, amesema kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kufanikisha juhudi za kuzuia na kutokomeza vitendo vya uhalifu katika eneo hilo.

Mkaguzi msaidizi wa Polisi Willy Lupa ambaye ni Polisi kata wa kata ya Nyamnyusi, Picha Hagai Ruyagila

Ameongeza kuwa tayari wamejipanga kuweka mikakati madhubuti ikiwemo kufanya dolia za mara kwa mara kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji na kata, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na Wanamgambo wa kata hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo.

Sauti ya Mkaguzi msaidizi wa Polisi Willy Lupa