Joy FM
Joy FM
27 March 2026, 17:43

Kuchangia damu ni tendo la kibinadamu lenye umuhimu mkubwa katika jamii yoyote ile na upatikanaji wake wa kutosha unaweza kuwa tofauti kati ya maisha na kifo kwa wagonjwa wengi.
Na Lucas Hoha
Wanachuo wa chuo cha ufundi Stadi Veta Kigoma wanaojifunza udereva wamejitolea kuchangia damu ili kusaidia na kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha hospitali kwa kukosa damu wakiwemo akina mama wajawazito na waliopata ajali.

Wakizungumza na Radio Joy baadhi ya wanafunzi waliochangia damu wamesema wao ni wahanga wa matukio ya ajali za barabarani, hivyo wameamua kuchangia ili kurudishia fadhila kwa jamii na kuokoa maisha ya wananchi wanaopoteza maisha.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa wanafunzi hao John Luganga amesema uwepo wa damu ya kutosha hospitali ni Mhimu, nakuwa wameamua kuhamasisha wanafunzi kuchangia ili kupunguza uhaba wa damu hospitali, huku Balozi wa usalama barabarani Mkoa wa Kigoma akipongeza wanafunzi hao kwa kujitolea.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Edward Elias amesema chuo hicho kinatoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma kuendesha vyombo vya moto tofautitofauti, huku akiwataka vijana kujiunga kusomea fani hiyo ili waweze kujiari.