Joy FM
Joy FM
27 March 2026, 11:12

Wananchi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wameiomba serikali kupitia TARURA kuboresha barabara zote za mitaani ili ziweze kupitika kwa urahisi ili ziweze kuchochea maendeleo kupitia shughuli za usafirishaji
Na Mwandishi wetu
Seikali imeanza kuchukua hatu za kujenga barabara za mitaani kwa kiwango cha lami nzito katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya miundombinu ya barabara pamoja na tope pamoja na vumbi, ambapo wananchi wameomba mkandarasi kusimamiwa ili mradi ukamilike kwa wakati.

Wilaya ya Kibondo ina asili ya udongo mwekundu, ambapo kwa wageni, nyakati za masika hukutana na tope la kutosha, huku kiangazi ukikutana na vumbi kero zilizowatesa wananchi kwa kipindi kirefu, kilio ambacho kimeanza kutatuliwa mara baada ya kuanza ujenzi wa barabara za mitaani kwa kiwango cha lami, ikiwa ni hatua kubwa ya maendelea na wananchi wakitoa shime kwa serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hizo.
Katika hatua nyingine wananchi wameomba barabara za kuingia stendi ya mabasi kufanyiwa kazi pia ili njia hizo zipitike bila shida, kwani mabasi yamekuwa yakikwama mara kwa mara kutokana na wingi wa tope nyakati za masika.

Meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA Wilaya ya Kibodo Mhandisi Dickson Kanyankole, amesema wanaendela kuchukua hatua za kuongeza mtandao wa barabara za lami, ili kuhakikisha hadhi ya mji wa kibondo unakuwa kwa kasi.