Joy FM

Wafanyabiashara wapongeza ujenzi wa soko Kibondo

25 March 2026, 09:53

Muonekano wa vibanda vya soko la samaki mjini Kibondo, Picha na Tryphone Odace

Halmashauri zina jukumu muhimu katika kusimamia na kuendeleza maeneo ya biashara kama vile masoko kama moja ya hatua muhimu zinazoweza kuchukuliwa ili kuinua hali ya wafanyabiashara na uchumi wa jamii na serikali  kwa ujumla na maboresho haya yanaweza kujumuisha ujenzi wa miundombinu bora, kuongeza usafi, pamoja na kuimarisha usalama wa eneo la soko.

Na Tryphone Odace

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko kuu Mjini Kibondo wameeleza kufurahishwa na ujenzi wa soko la samaki ambalo kukamilika kwake kutasaidia kuondoa changamoto za wafanyabiashara kuuuzia bidhaa zao katika mazingira ambayo si rafiki.

Wakizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibondo walipotembelea mradi wa soko ambao unajengwa kwa kutumia mapato ya ndani wamesema awali walikuwa wakisumbuliwa na mvua na jua na kusababisha bidhaa zao kuharibika.

Sauti ya wafanyabiashara Kibondo
Muonekano wa vibanda vya soko la samaki mjini Kibondo, Picha na Tryphone Odace

Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya miundombinu Halmashauri ya Wilaya Kibondo Edwin Edward amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2024 na lengo ni kuweka soko hilo kuwa la kisasa kwa wafanyabiashara.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Idara ya miundombinu Halmashauri ya Wilaya Kibondo Edwin Edward
Kaimu Mkuu wa Idara ya miundombinu Halmashauri ya Wilaya Kibondo Edwin Edward, Picha na Tryphone Odace

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Steven Jankis amesema mradi huo unalenga kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri kwa kuwaboreshea wafanyabiashara mazingira ya kufanyia kazi na kuwa soko hilo litakamilika june 31 mwaka huu.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Steven Jankis