Joy FM

Upatikanaji wa maji Buhigwe ni 84.3%

21 March 2026, 14:07

Muonekano tanki la maji katika mradi wa maji wa Mnanila – Nyakimwe Wilayani Buhigwe, Picha na Tryphone Odace

Maji ni rasilimali muhimu katika maisha ya binadamu na viumbe hai kwa ujumla na ustawi wa jamii umehusishwa moja kwa moja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa afya ya binadamu kwa waananchi wanapopata maji safi na salama, huweza kuepuka magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, kuhara, na homa ya matumbo

Na Tryphone Odace

Serikali  kupitia RUWASA Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma imefanikiwa kusambaza maji katika vijiji nane ambavyo vilikuwa havina huduma ya maji baada ya mradi wa maji wa Mnanila – Nyakimwe kukamlika ambao unatajwa kupunguza adhaa ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.

Akizunumza na Redio Joy Fm, ilipotembelea mradi huo wa maji wa Mnanila – Nyakimwe,  Fundi sanifu mwandamizi kutoka RUWASA Buhigwe ambaye pia ndie Msimamizi wa mradi huo Mhandisi  Frnsis John Mollel amesema  mradi huo utahudumia wananchi waliokuwa wakilazimika kutumia maji ya mito.

Sauti ya Fundi sanifu mwandamizi kutoka RUWASA Buhigwe ambaye pia ndie Msimamizi wa mradi huo Mhandisi  Frnsis John Mollel
Muonekano wa taki la maji katika mradi wa maji wa Mnanila – Nyakimwe Wilayani Buhigwe, Picha na Tryphone Odace

Mhandisi  Marwa  amesema  hali ya upatikanaji wa maji imeendelea kuimarika na kuwa kufikia mwezi June mwaka huu wananchi wote watakuwa wanapata huduma ya maji kwa uhakika.

Sauti ya Fundi sanifu mwandamizi kutoka RUWASA Buhigwe ambaye pia ndie Msimamizi wa mradi huo Mhandisi  Frnsis John Mollel

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wamepongeza hatua ya serikali kuwapelekea mradi wa maji kwani utawasaidia kuepukana na matumizi ya maji ya mito ambayo yalikuwa si salama kwa afya zao.

Sauti za wananchi Buhigwe

Mpaka sasa hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri ya Wilaya Buhigwe Mkoani Kigoma ni asilimia  84.3 na kuwa utekezaji wa miradi ya maji unaoendelea kufanywa na seriakali itakuwa chachu ya kumaliza hali ukosefu wa maji kwa wananchi wilayani humo.