Joy FM

Viongozi watakiwa kusimamia urejeshaji wa mikopo ya 10% Kasulu

18 March 2026, 13:42

Baadhi ya watendaji wa kata na mitaa wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Urejeshwaji wa mikopo inayotolewa na Halmashauri unasidia kuweza kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo mingine kwa vikundi vingine vyenye uhitaji wa mikopo

Na Hagai Ruyagila

Watendaji wa kata na Mitaa halmashauri ya mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia na kufuatilia kwa karibu urejeshwaji wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa wananchi kupitia Halmashauri mbalimbali Nchini.

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akizungumza na viongozi wa kata na mitaa, Picha na Hagai Ruyagila

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa halmashauri ya Mji Kasulu katika kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu yao ya Kila siku

Kanal Mwakisu amewasisitiza umuhimu wa watendaji hao kuwa karibu na Wananchi katika maeneo yao ili waweze kutoa elimu kuhusu ulazima wa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati, badala ya kusababisha hasara kwa halmashauri.

Aidha, Kanali Mwakisu ameeleza kuwa iwapo mikopo itatokewa kwa watu wasiokuwa na sifa stahiki, watendaji husika wanapaswa kuwajibika kwa uzembe huo.

Kwa upande wake, Afisa mwandamizi wa TAKUKURU kutoka dawati la uchunguzi wilaya ya Kasulu Alfa Eliyatosha, ameeleza wajibu wa watumishi wa umma katika kuzuia vitendo vya rushwa, akisisitiza uwajibikaji na uadilifu katika utendaji kazi wao.

Afisa mwandamizi wa TAKUKURU kutoka dawati la uchunguzi wilaya ya Kasulu Alfa Eliyatosha, Picha na Hagai Ruyagila

Naye, afisa mtendaji wa mtaa wa Sinza, kata ya Mwilamvya, Njile Charles, akizungumza kwa niaba ya watendaji wenzake, amesema watahakikisha wanafuatilia kwa karibu urejeshwaji wa mikopo hiyo ili kuepuka upotevu wa fedha na kuilinda serikali dhidi ya hasara.