Joy FM

DC Kigoma apongeza serikali kuimarisha upatikanji wa umeme

17 March 2026, 15:59

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akiwa kwenye picha na viongozi wa TANESCO wakati wa hafla ya kugawa vyombo vya moto, Picha na Mwandishi wetu

Vitongoji 316 Mkoani Kigoma vinatarajia kupata umeme  ambapo serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 54 ili kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Kigoma, na kwamba hatua hiyo imechangia pakubwa kusukuma mbele kasi ya maendeleo ya mkoa huo.

Amesema kwa miaka mingi Wilaya ya Kigoma na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla umekuwa ukipata changamoto kubwa ya umeme iliyotokana na kutounganishwa kwenye gridi ya Taifa, lakini chini ya serikali ya awamu ya sita changamoto hiyo imebaki kuwa historia tu.

Baadhi ya vyombo vya moto vilivyokabidhiwa kwa TANESCO Kigoma, Picha na Mwandishi wetu

Dkt. Chuachua, amesema hayo leo Machi 17, 2026 wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye hafla fupi ya kupokea na kukabidhi magari matano, Bajaji tano na Pikipiki kumi na moja kwa Mameneja wa TANESCO kutoka Wilaya zote za mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chua

Aidha Dkt Chuachua amesema kwa kuwa na usafiri imara TANESCO, itaweza kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na kutatua changamoto za huduma ya umeme kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akikata utepe wakati wa kukabidhi vyombo vya moto TANESCO, Picha na Mwandishi wetu

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Hassan Nganjau, akiongea mara baada ya kukabidhiwa magari, Bajaji na Pikipiki, amesema yataleta tija kwa kurahisha utendaji kazi wao.

Sauti ya Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Hassan Nganjau,

Akiongea kwa niaba ya Mameneja wezake Kaimu Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kakonko Mercy Mwanga amesema upatikanaji wa usafiri unaenda kutatua changomoto za kuchelewa kufika kutatua changamoto zinazokuwa zimejitokeza kwa wananchi.

Sauti ya Mameneja wezake Kaimu Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kakonko Mercy Mwanga