Joy FM
Joy FM
16 March 2026, 12:11

Utunzaji wa mazingira ni jambo muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe wengine duniani na katika miaka ya hivi karibuni, dunia imekumbwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi ambayo imesababisha mabadiliko ya hali ya hewa kama vile ukame, mafuriko na ongezeko la joto duniani.
Na Mwandishi wetu
Baadhi ya waoteshaji wa miti ya kutunza mazingira Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya upandaji wa miti itakayosaidia katika kutunza mazingira na kupunguza hewa ukaa.
Hayo yameelezwa na Bw. Eliakimu Bitabo pamoja na Bi. Seili Eliakimu wakati wakiongea na Redio Joy Fm kwenye bonde la kijiji cha Kumwambu kata ya Kumwambu
Wamesema upandaji wa miti husaidia kuzuia ongezekola hewa ukaa na kuongeza kinga dhidi ya mafuriko na mmomonyoko wa udongo hasa maeneo yenye mwinuko.
Hata hivyo mpango wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo ni kupanda miti milioni 1 na laki 5 kila mwaka kutoka kwenye vitalu vya wakala wa huduma za misitu TFS ambao wamekuwa wakiwagawia wananchi miti ya kupanda kwenye maeneo yao.