Joy FM

Waaswa kutenda mema kipindi cha kwaresma Kasulu

13 March 2026, 12:58

Mchungaji Bhikolimana Abrahamu Bhitona, Picha na Hagai Ruyagila

Mchungaji Bhikolimana Abrahamu Bhitona

Katika msimu huu wa mfungo wa Kwaresma, Waumini wa Dini ya Kikristo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameaswa kuendelea kutenda matendo mema ili kuenzi mateso na kifo cha Yesu Kristo pamoja na kuimarisha upendo na mshikamano katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mchungaji Bhikolimana Abrahamu Bhitona kutoka Kanisa la Anglikana lililopo Mjini Kasulu wakati akizungumza na radio Joy fm.

Amesema ni vyema kutenda mema wakati huu na baada ya mfungo wa Kwaresma ili kudumisha matendo ya huruma, kusaidia wahitaji, na kuishi maisha yanayompendeza Mungu kila siku, si kwa kipindi hiki tu bali hata baada ya Pasaka.

Sauti ya Mchungaji Bhikolimana Abrahamu Bhitona kutoka Kanisa la Anglika

Aidha, Mchungaji Bhitona amesema unapofunga katika msimu huu ni vizuri kuomba rehema kwa kumrudia Mungu ili aweze kusaheme dhambi, kuimarisha imani, na kukupa nguvu ya kushinda majaribu.

Sauti ya Mchungaji Bhikolimana Abrahamu Bhitona kutoka Kanisa la Anglika

Baadhi ya waumini wa Dini ya Kikristo wilayani Kasulu wamesema msimu wa Kwaresma umekuwa ni fursa ya kutafakari maisha yao, kusaidiana na wenye uhitaji, pamoja na kuimarisha mahusioano yao na Mungu kwa njia ya sala na matendo mema.

Sauti ya waumini wa Dini ya Kikristo