Joy FM

Kibondo wahimizwa kutumia majiko sanifu

13 March 2026, 08:29

Mkuu wa Wilaya Kibondo akiwa na Mkurugenzi wa Tanzanzania Women  Empowerment Network wakati wa kugawa majiko banifu, Picha na Dotto Josephati

Majiko sanifu ni majiko yaliyoboreshwa ili kutumia nishati kama kuni au mkaa kwa ufanisi zaidi na katika jamii nyingi, hasa maeneo ya vijijini na mijini, majiko haya yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa maisha ya wananchi kwani majiko sanifu huchangia katika kuboresha maisha ya watu kiuchumi, kiafya na kimazingira.

Na Dotto Josephati

Wananchi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa kuchangamkia fursa ya kununua majiko sanifu yanayotumia mkaa kidogo ili iweze kuwapunguzia gharama za kutumia kuni na mkaa ambapo majiko hayo yana ruzuku ya serikali kwa asilimia 85.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza wakati wa uzinduzi wa majiko hayo katika Kata ya Nyaruyoba ambayo yametengezwa na kampuni ya INVOTEC na kusambazwa na REA  ambapo amewahimiza wananchi watakaopata majiko hayo kuyatumia vizuri ili yaweze kuwasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza
Mkuu wa Wilaya Kibondo na viongozi wengine wakigawa majiko banifu kwa wanawake, Picha na Dotto Josephati

Naye mkurugenzi wa taasisi ya Tanzanzania Women  Empowerment Network Bi. Frolence Masunga amesema lengo kuu la kutoa majiko hayo ni kumsaidia mwananchi kuepukana na magonjwa yanatokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia na kuendelea kulinda afya za watanzania.

Sauti ya mkurugenzi wa taasisi ya Tanzanzania Women  Empowerment Network Bi. Frolence Masunga
Mkuu wa Wilaya Kibondo na viongozi wengine wakigawa majiko banifu kwa wanawake, Picha na Dotto Josephati

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka REA Bw. Ramadhan  Ramadhan amesema majiko hayo yana ubora wa hali ya juu ambalo litamsaidia mwananchi kutumia mkaa kidogo na wanaendelea kuhamasisha wananchi kutumia mkaa mbadala kwaajili ya kuendelea kutunza mazingira.

Sauti ya Mwakilishi kutoka REA Bw. Ramadhan  Ramadhan