Joy FM

Mradi wa KITIKI waongeza uzalishaji wa mazao Kasulu

12 March 2026, 15:02

Shamba darasa kutoka kikundi Cha wakulima Cha nyanguge kata ya Nyumbigwa Halmashauri ya Mji Kasulu Picha na Hagai Ruygaila

Mkoa wa Kigoma umefanikiwa kupunguza kiwango cha upotevu wa mazao wakati na baada ya kuvuna kutoka asilimia 11% mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 8%, ya sasa.

Na Hagai Ruyagila

Wakulima wa Kata ya Nyumbigwa katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wamesema uwepo wa Mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KITIKI) umesaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya mahindi alizeti na maharage kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.

Mradi wa Kilimo Tija Kigoma KITIKI unafadhiliwa na serikali ya korea kusini KOICA na kutekelezwa na mashirika ya world vision Tanzania na Goodneighbors chini ya usimamizi wa shirika la Mpango wa chakula Duniani (WFP) na unatekelezwa katika halmashauri ya mji kasulu, halmashauri ya wilaya ya Kibondo, halmashauri ya wilaya ya Kasulu na halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Kikundi Cha wakulima nyanguge kutoka kata ya Nyumbigwa Halmashauri ya Mji Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Mradi huo umeendelea kuleta matokeo chanya katika uzalishaji na kuongeza kipato cha mkulima kama wanavyoeleza wakulima kutoka kikundi cha wakulima nyanguge kata ya nyumbigwa wakati wa maadhimisho ya siku ya mkulima shambani.

Sauti za wakulima

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mwakilishi wa Meneja wa Mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KITIKI) Samson Katabila amezungumzia namna mradi huo ulivyoweza kuwanufaisha wakulima zaidi ya elfu 19 Katika halmashauri zote ambako mradi huo unatekelezwa lengo ikiwa ni kuhakikisha wakulima wanapata manufaa kupitia mazao wanayozalisha.

Sauti ya Mwakilishi wa Meneja wa Mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KITIKI) Samson Katabila
Mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi wa Diwani wa kata ya Nyumbigwa ndugu Yasini Ntimanya akitembelea mazao yanayozalishwa kupitia mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KITIKI), Picha na Hagai Ruyagila

Kaimu Mkuu wa kitengo cha Kilimo mifugo na Uvuvi halmashauri ya Mji Kasulu Zephania Sodya amewataka wakulima waliopatiwa mafunzo kutoa elimu kwa wakulima wengine ili waachane na kilimo cha mazoea ili kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha Kilimo mifugo na Uvuvi halmashauri ya Mji Kasulu Zephania Sodya
Kaimu Meneja wa mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KITIKI) Samson Katabila akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi, Picha na Hagai Ruyagila

Mwakilishi wa Diwani wa kata ya Nyumbigwa, Yasini Ntimanya amewasihi wakulima kuendelea kutumia mafunzo hayo kuongeza uzalishaji wa mazao.

Sauti ya Mwakilishi wa Diwani wa kata ya Nyumbigwa, Yasini Ntimanya
Mwakilishi wa Diwani wa kata ya Nyumbigwa ndugu. Yasini Ntimanya, Picha na Hagai Ruyagila