Joy FM
Joy FM
11 March 2026, 12:53

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na Kwaresma kwa wakristo viongozi wa dini hawana budi kuendelea kuwaunganisha waumini wao ili kuweza kuishi kwa upendo
Na Hagai Ruyagila
Viongozi wa dini wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuhubiri amani, upendo na mshikamano kwa waumini wao ili kudumisha hali ya utulivu na umoja katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu wakati akizungumza katika hafla ya iftari iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kushirikiana na shirika la Posta Tanzania ikiwakutanisha viongozi mbalimbali wa dini wilayani humo.

Kanali mwakisu Amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta migogoro au kuvuruga utulivu wa nchi.
Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Kasulu Shekhe Ruhettah Ahmad Hussein amesema mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa muhimu kwa waumini kuimarisha ibada, kusaidiana na kudumisha amani, huku akiwataka waumini kuwa na umoja katika jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Kasulu