Joy FM
Joy FM
9 March 2026, 12:48

Watoto wenye mahitaji maalum ni watoto ambao wanahitaji msaada wa ziada katika maisha yao ya kila siku kutokana na changamoto za kimwili, kiakili au kijamii kutokana na kuwa watoto hawa ni sehemu ya jamii na wana haki sawa kama watoto wengine ya kuwasaidiwa na kupata mahitaji maalum.
Na Dotto Josephati
Mtandao wa wanawake Polisi Wilaya ya Kibondo (TPF-NET) wametoa msaada wa vitu mbali mbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Nengo vitakavyo wasaidia wanapokuwa shuleni ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo kwa kuwasaidia watu wenye mahitaji
Zawadi hizo walizotoa ni sehemu ya kufanya matendo ya huruma kuelekea siku ya wanawake duniani ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Mkaguzi Aneth Colman Mlema amesema lengo kuu la kufanya matendo ya huruma ni kuwafanya watoto hao kutojiona wapweke na kuendelea kuwapatia furaha.

Kwaupande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Ibrahimu Alfred amewashukuru wanawake hao kwa msaada huo walioutoa huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia kwani shule hiyo ina uhutaji mkubwa
Shule ya msingi Nengo ina jumla ya wanafunzi 700 ambapo wanafunzi wenye ulemavu ni wanafunzi 146 ambapo mtandao wa wanawake Polisi Wilaya ya Kibondo wameatembelea shule hiyo ns kutoa msaada wa sabuni, Mchele, yebo yebo, juisi biskuti ambavyo vimegharimu shilling laki nane