Joy FM

Vikundi 142 vya wanawake vyanufaika na mikopo Kasulu

9 March 2026, 12:32

Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi Theresia Mtelewe, Picha na Hagai Ruyagila

Mikopo ni fedha zinazotolewa na taasisi za kifedha au mashirika mbalimbali kwa watu binafsi au vikundi ili kuwasaidia kuanzisha au kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa wanawake huunda vikundi maalum ili kupata mikopo kwa urahisi zaidi.

Na Hagai Ruyagila

Zaidi ya wanawake elfu 1 kutoka vikundi 142 Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamenufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo inatajwa  kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Mikopo hii inalenga kuwanufaisha wanawake, vijana na watu wenye mahitaji Maalumu ambayo huwasaidia kujikwamua kiuchumi katika kufikia malengo yao ya baadaye.

Baadhi ya wanawake waliohudhuria katika maadhimisho hayo, Picha na Hagai Ruyagila

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa wilaya ya Kasulu yamefanyika usiku wa March 7 mwaka huu Katibu tawala wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele amebainisha namna mikopo hiyo inavyowanufaisha wanawake katika wilaya hiyo.

Sauti ya Katibu tawala wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele

Akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amepongeza mwitikio wa wanawake katika kuchangamkia fursa na kutoa rai kuhakikisha fedha hizo zinaleta tija katika shughuli zao za uzalishaji mali.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wanawake wilayani Kasulu wameeleza mitazamo yao kuhusu mikopo hiyo na namna inavyoweza kuwanufaisha.

Sauti ya Baadhi ya wanawake