Joy FM

Wafanyabiashara walia ukosefu wa soko Kazuramimba Uvinza

5 March 2026, 12:29

Baadhi ya wafanyabiashara wa Kazuramimba wakiendelea na biashara kando na barabara, Picha na Orida Sayon

Serikali katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma imesema imeanza utekeleza wa ujenzi wa soko la Kazuramba umeanza ili kujenga soko litakalosaidia wafanyabiashara

Na Orisa Sayon

Wafanyabiashara wadogo katika soko la Kazurumimba Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza
Mkoani Kigoma wameomba kujengewa sehemu maalumu ya kufanyia biashara zao ili
kuondokana na adha ya kufanya biashara pembezoni mwa barabara.

Wafanya biashara wadogo wa bidhaa mbalimbali sokoni hapo wanapitia adha ya kukosa eneo
maalumu ya kufanyia biashara hali inayopelekea kupanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara
inayotumika kwa usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa kutoka mkoani kigoma kwenda mikoa
mingine ambapo wamedai hali hiyo inahatarisha usalama wao.

Sauti ya wafanyabiashara

Akizungumza na kituo hiki Diwani wa kata ya Kazuramimba Mhe, Mussa Chessa Mpangilio
mbovu wa soko hilo ni miongoni mwa sababu kubwa inayochangia wafanyabiashara wengi
kukosa maeneo sahihi na muhimu kwa ajili ya kupanga na kuuza bidhaa zao.

Wafanyabiashar katika soko la Kazuramimba Wilayani Uvinza, Picha na Orida Sayon

Amesema uongozi wa kata hiyo upo katika uandaaji wa mkakati wa kujenga soko hilo na
ametumia nafasi hiyo kukalibisha wawekezaji kujitokeza katika uwekezaji wa soko ili
kurahisisha zoezi hilo kwa lengo la kuwaondoa wafanyabiashara pembezoni mwa barabara.

Akijibia Kero hiyo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe, Dinna Mathani amesema tayari utekelezaji
wa ujenzi wa eneo maalumu la kufanyia biashara upo kwenye mkakati na baada ya miezi
michache watajengewa vibanda vitakavyowawezesha kuepuka kufanya biashara pembezoni mwa
barabara.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe, Dinna Mathani