Joy FM
Joy FM
4 March 2026, 16:51

Ushiriki wa wananchi katika kukemea vitendo vya ukatili ni msingi muhimu wa kujenga jamii salama, yenye haki na usawa na wanaposhiriki kikamilifu, husaidia kuzuia uhalifu, kulinda waathirika, na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
Na Mwandishi wetu
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, amewataka wananchi kuhakikisha wanapinga matukio ya ukatili hasa ubakaji na ulawiti, ambayo yamepelekea wanawake wengi kuathirika.
Katika taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Sirro, iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu tawala Mkoa Hassan Rugwa, amesema maadhimisho ya wanawake kimkoa yatafanyika Kasanda Wilayani kakonko, na kwamba ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha anapinga matukio yaliyopo ndani ya jamii ili kuongeza ustawi wa raia.
Kwa upande wake, Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Kigoma Msafiri Nzunuri, amesema licha ya wananchi kuripoti matukio hayo ili kupatiwa ufumbuzi wa kisheria, bado yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara, ambapo amesisitiza hatua zichukuliwe ili jamii kubaki salama.
