Joy FM

Wakristo watakiwa kusaidia wenye uhitaji Buhigwe

24 February 2026, 16:30

Baadhi ya Waumini wa kanisa la Mtakatifu Paulo Anglikana Kitambuka wilayani Buhigwe, Picha na Hagai Ruyagila

Kwaresma ni wakati wa kuonyesha imani kwa vitendo kwa kuwasaidia wenye uhitaji kupitia matendo ya huruma na upendo.

Na Hagai Ruyagila

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika, Mhashamu Emmanuel Bwatta, amewataka waumini wa dini ya Kikristo mkoani Kigoma kutumia kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma kuwakumbuka na kuwasaidia watu wenye uhitaji, hususan watoto waliopo katika vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji.

Askofu Bwatta ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Mtakatifu Paulo Anglikana Kitambuka lililopo Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika, Mhashamu Emmanuel Bwatta, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema Kwaresma ni kipindi maalum cha kutafakari, kutubu na kutenda matendo ya huruma kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika, Mhashamu Emmanuel Bwatta,

Ameongeza kuwa kufanya matendo mema, ikiwemo kutoa msaada kwa wahitaji, ni njia mojawapo ya kuonesha upendo wa kweli na kumtii Mungu, jambo ambalo huleta baraka na mafanikio katika maisha ya mwanadamu.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika, Mhashamu Emmanuel Bwatta,

Kwa upande wao, baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo mkoani Kigoma wamesema kuwasaidia wahitaji ni jukumu la kila muumini, wakisisitiza kuwa matendo hayo huleta baraka za moja kwa moja kutoka kwa Mungu na kuimarisha mshikamano katika jamii.

Sauti ya baadhi ya waumini