Joy FM

Wakristo watakiwa kuhubiri amani kuimarisha maendeleo Kasulu

19 February 2026, 15:57

Mchungaji Kiongozi wa kanisa la CGRA Dickison Nyandura, Picha na Hagai Ruyagila

Amani na mshikamano ni nguzo ya maendeleo endelevu na kila mwananchi ana wajibu wa kulinda amani kwa matendo na maneno yake.

Na Hagai Ruyagila

Waumini wa dini ya Kikristo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, wametakiwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili kuimarisha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi Dickison Nyandura, wa Kanisa la CGRA lililopo Kata ya Murusi halmashauri ya Mji Kasulu wakati akizungumza na redio cha Radio Joy FM Februari 19.

Mchungaji Nyandura amesema amani ni msingi muhimu wa maendeleo, akieleza kuwa taifa lenye utulivu hujenga mazingira bora ya uwekezaji, utoaji wa huduma za kijamii na ustawi wa wananchi wake.

Ameonya kuwa kukosekana kwa amani kunaweza kusababisha migogoro na kuvuruga mshikamano wa kijamii.

Sauti ya Mchungaji Kiongozi Dickson Nyandura, wa Kanisa la CGRA

Aidha, Mchungaji Nyandura amewahimiza waumini pamoja na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuombea taifa, kuheshimu sheria za nchi na kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa moyo wa upendo na umoja.

Sauti ya Sauti ya Mchungaji Kiongozi Dickson Nyandura, wa Kanisa la CGRA

Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo wilayani Kasulu wameunga mkono wito huo, wakisema kuwa amani imekuwa chachu ya maendeleo katika eneo hilo na kwamba wako tayari kushirikiana na viongozi wa dini na serikali kuhakikisha utulivu unaendelea kudumishwa.

Sauti ya waumini

Kudumisha amani si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi ili kulinda ustawi na maendeleo ya taifa.