Joy FM
Joy FM
13 February 2026, 14:54

Halmashauri ya Mji wa Kasulu kupitia baraza la madiwani lililo keti hivi karibuni walikubaliana kukusanya na kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi billion 40 kwa mwaka wa fedha 2026/27 hivyo oparesheni hiyo ni moja na mwanzo kwa halmashauri hiyo kukusanya na kusimamia vyema vyanzo mapato.
Na Emmanuel Kamangu
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwa kushirikiana na maafisa biashara sambamba na wataalamu wa tehama katika halmashauri hiyo wamefanya oparesheni maalumu ya kukagua leseni kwa wafanyabiashara.
Oparesheni hiyo ambayo imechukua takribani saa 13 katika soko la kimkakati la mazao Mnadani liliko Kata ya Kigondo Halmashauri ya Mji wa Kasulu imelenga kutoa elimu kwa wafanya biashara juu ya kulipa kodi kwa hiyari.
Akihitimisha oparesheni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye akutumia mwanya huo kuwasihi wafanyabiashara wenye sitoo za mazao pamoja na wafanya biashara wa bidhaa mbali mbali kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa wakati ili kuharakisha maendeleo ya halmashauri hiyo.
Aidha Mwl Simbeye amesema serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani imeendelea kuweka mazingra wezeshi na rafiki kwa mfanyabiashara ili kuwasaidia kukua na kuendelea kiuchumi hivyo hakuna sababu za kukwepa kulipa kodi.
Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara katika Halmashauri ya mji wa Kasulu wamempongeza Mkurugenzi Simbeye kwa kusimamia swala la mapato ya Halmashauri kikamilifu jambo linaloonyesha dhamira njema ya kuharakisha maendeleo katika halmashauri hiyo.