Joy FM

DED Kasulu ahimiza nidhamu kwa walimu na wanafunzi kuongeza ufaulu

13 February 2026, 14:15

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu mwl Vumilia Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma imewataka walimu wakuu wa shule za Sekondari kuhakikisha wanasimamia nidhamu ili kuongeza ufaulu

Na Hagai Ruyagila

Wakuu wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia suala la nidhamu kwa waalimu na wanafunzi ili kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu mwl Vumilia Simbeye wakati Akifungua kikao cha awali cha umoja wa wakuu wa Shule TAHOSSA chenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la taaluma na nidhamu shuleni.

Mwl Simbeye amesisitiza kusimamia ipasavyo mienendo ya nidhamu kwa waalimu na wanafunzi Pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu mwl Vumilia Simbeye
Baadhi ya walimu wakiwa katika mkutano ambao umeendeshwa na Mkurugenzi wa Kasulu Mji, Picha na Hagai Ruyagila

Aidha ameongeza kwa kuwataka wakuu wa shule kushirikiana na wazazi kudhibiti suala la utoro pamoja na kukemea tabiaa za baadhi ya waalimu wanaofanya shughuli binafsi muda wa vipindi darasani.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu mwl Vumilia Simbeye

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule ambao wameshiriki kikao hicho, Mkuu wa shule ya Sekondari Kigoma Gland Mwl Severino manyota wamehiadi kutekeleza na kusimamia maagizo hayo.

Sauti ya Mkuu wa shule ya Sekondari Kigoma Gland Mwl Severino
Mkuu wa shule ya Sekondari Kigoma Gland Mwl Severino, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wananchi wameeleza matarajio na manufaa yao ikiwa waalimu hao watasimamia nidhamu shuleni pamoja na kudhibiti suala la utoro kwa waalimu na wanafunzi.

Sauti za wananchi