Joy FM
Joy FM
6 February 2026, 12:30

Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuhimiza wajibu wa msingi na wa kudumu wa kwa wananchama wake ili kuhakikisha CCM inakuwa chama cha Watanzania na kimbilio lao.
Na Hagai Ruyagila
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Mhe, Dkt Mwigulu Nchemba amewataka wananchi mkoani Kigoma kudumisha amani ili kuendelea kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na mamia ya wafuasi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya chama hicho katika uwanja wa Kiganamo Mjini Kasulu, Akiwa amemuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) Christopher Gachuma amesisitiza suala la kudumisha amani kwa wananachi.
Aidha Gachuma amewataka watumishi wa umma mkoani Kigoma kusimamia kikamilifu fedha za serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ameahidi kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote ya mkoa huo.
Maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mkoa wa Kigoma yamefanyika Wilayani Kasulu yakiwa yamebebwa na kauli mbiu isemayo. ”Tumechagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa letu”