Joy FM

World vision yakabidhi miradi ya bilioni 1.47 Kakonko

5 February 2026, 16:43

Nembo ya shirika la World Vision, Picha na Mtandao

Miradi inayotekelezwa na mashirika ya kimataifa ina umuhimu mkubwa sana kwa wananchi hasa kwa kuzingatia hali ya kijamii, kiuchumi na kijiografia.

Na Mwandishi wetu

Shirika la World vison limekabidhi miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.47 wilayani Kakonko ikiwemo mradi wa maji ambapo zaidi ya wananchi elfU 4000 wanatarajia kunufaika na mradi wa maji Nyamwironge wilayani Kakonko.

Akizungumza wakati wa kukabidhi miradi hiyo, Meneja wa World Vision kanda ya magharibi Jacqueline Kaihura amesema miongoni mwa miradi ambayo imekabidhiwa ni pamoja na mradi wa maji ambao unatajwa kwenda kuwanufaisha wananchi wa maeneo hayo kwani tanki ambalo limejengwa lina uwezo wa kuhifadhi lita zaidi ya elf 50.

Sauti ya Meneja wa World Vision Kanda ya Magharibi Jacqueline Kaihura

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa pamoja na Kaimu mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kakonko wamewataka wadau wengine kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo wilayani humo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa

Naye Denis Manji ambae ni mtaalam wa maji RUWASA Kakonko amesema ujio wa mradi huo utasaidia wananchi kupata maji safi na salama na kupunguza changamoto ya uwepo wa magonjwa ya tumbo kwa wananchi.

Sauti ya Denis Manji ambae ni mtaalam wa maji RUWASA Kakonko

Wananchi nao wanalishukuru shirika la World Vision kwani hapo awali walilazimika kufuata huduma ya maji vijiji jirani na muda mwingine walilazimika kutumia maji yasio safi na salama.

Sauti ya Wananchi

Mradi mwingine uliokabidhiwa ni pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo matundu 10 ya wasichana na wavulana kwenye shule 3 pamoja na chumba maalum kwa ajili watoto wakike kujistiri wakati wa hedhi, sambamba na vyoo kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.