Joy FM

Baraza la madiwani lapitisha bajeti ya zaidi ya bilioni 43 Kasulu

5 February 2026, 10:23

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh Ayubu Ngalaba, Picha na Hagai Ruyagila

Bajeti hiyo imepitishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026 Oktoba, Novemba na Desemba ikiwa na lengo la kuhakikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo itakayogusa na kuboresha maisha ya wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu.

Na Hagai Ruyagila

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma limepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 43 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha uliopita 2025/ 2026.

Madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa kwenye kikao Cha baraza la Madiwani, Picha na Hagai Ruyagila

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mh. Ayubu Ngalaba amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuziba mianya ya upotevu wa mapato ili kuhakikisha halmashauri hiyo inafikia lengo ya bajeti iliyokusudiwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mh. Ayubu Ngalaba

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye amesema halmashauri imepokea maoni na marekebisho yote yaliyopendekezwa na baraza, na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inatekelezwa kwa wakati na bila changamoto.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele akitoa salamu za serikali kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Kanal Isaac Mwakisu katika kikao cha baraza la madiwani amesema serikali imeandaa bima ya afya kwa wananchi wote nchi ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo awamu ya kwanza wananchi watagharamiwa na serikali na awamu ya pili wanchini watachangia.

Sauti ya Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtelewe, Picha na Hagai Ruyagila

Nao baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa utekelezaji mzuri wa bajeti hiyo ndio msingi wa maendeleo ya Halmashauri ya Mji Kasulu, wakisisitiza umuhimu wa kuitekeleza kwa uadilifu, uwazi na kuzingatia thamani ya fedha kwa manufaa ya wananchi.

Sauti ya baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho
Madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa kwenye kikao Cha baraza la Madiwani, Picha na Hagai Ruyagila