Joy FM
Joy FM
28 January 2026, 12:53

Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Kasulu wametakiwa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kuwa na ubora unaokusudiwa
Na Emmanuel Kamangu
Mkuu wa Mkoa wa kigoma IGP Mstafu Balozi Simon Sirro amewataka madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuzingatia maadili ya utumishi pamoja kusimamia shuguli za maendeleo kikamilifu.
Balozi Sirro amebainisha hayo wakati akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ambapo amewataka kusimamia maendeleo ya wananchi kwa vitendo na kujitenga na rushwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.

Aidha Balozi siro amewataka madiwani kuhamasisha wananchi kujikita katka kilimo cha biashara ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isack Mwakisu amewaomba madiwani kutembea katika kile alichoelekeza balozi Siro hasa kwa kuendelea kuhakikisha wanannchi wao wanaendelea kupewa elimu ya kufuga na kulima kisasa.

Baadhi ya madiwani katika Halmashauri hiyo wameahidi kufanyia kazi maelekezo ya mkuu wa mkoa Balozi siro ili kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa uadirifu na kuwaletea maendeleo.