Joy FM
Joy FM
20 January 2026, 11:37

Maeneo ya hifadhi ni maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kulinda maliasili kama vile wanyamapori, mimea na mazingira kwa ujumla, maeneo haya yana mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira, kukuza utalii, na kulinda urithi wa taifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Shirika la TAWEA limesema linaendelea kukuza ujirani mwema baina ya wananchi wa vijiji vinne vinavyozunguka maeneo ya hifadhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ili kutatua migogoro ya wananchi na mamlaka za hifadhi ambazo zimekuwa zikijitokeza lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za Kilimo kwa uhuru.
Mara kwa mara kumeshuhudiwa malalamiko kadhaa kwa wananchi kuvamia na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo ya hifadhi pasipokuwa na vibali maalumu huku Wananchi nao wakilalamikia mamlaka za Usimamizi na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kutumia nguvu kuwaondoa katika maeno hayo.

Hatua hiyo imewaibua wadau wa maendeleo Shirika la Tanzania wote Equality Alliance (TAWEA) kupitia mradi wao wa uhifadhi wa Mazingira kuja na mpango wa kukuza ujirani mwema baina ya wananchi wa vijiji vya Kaburanzwili, Mvinza, kagerankanda na chekenya na mamlaka za uhifadhi wa misitu kama anavyoeleza Afisa mradi wa shirika hilo Bw. Batro Ngilangwa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha chekenya na kabulanzwili wanasema wanasubiri kuona mpango huo ukifanikiwa huku wakitoa wito kwa wananchi wenzao.
Afisa mtendaji wa kata ya Kagera nkanda Banyikwa John anasema kupitia kikao na makubaliano yaliyofikiwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuzingatia sheria na taratibu za namna ya kufanya shughuli katika maeneo ya hifadhi.

Afisa wanyamapori wilaya ya Kasulu Bw. Mohamed Omary anasema wananchi wanapaswa kuzingatia sheria kabla ya kuingia na kufanya shughuli katika maeneo ya hifadhi.