Joy FM
Joy FM
19 January 2026, 15:25

Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekanya ameupongeza wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Kigoma kwa kumsimamia vizuri mkandarasi anaejenga barabara ya Malagarasi-Ilunde- Uvinza kwa kuikamilisha kwa viwango.
Na Josephine Kiravu
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemwagiza mkandarasi STECOL anaejenga barabara ya Malagarasi –Ilunde –uvinza km 51.1 kwa kukamilisha ujenzi wa daraja la Ruchugi katika kipindi cha mwezi mmoja toka sasa ili lianze kutumika.
Hayo yamejiri wakati wa ziara yake ambapo pamoja na mambo mengine amekagua ujenzi wa barabara ya ya Tabora –kigoma ambapo ameupongeza uongozi wa TANROADS mkoa wa kigoma kwa kumsimamia vyema mkandarasi na kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ambyo inakwenda kuufungua mkoa kiuchumi.
Amesema Serikali imedhamiria kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami kila upande ili kuufanya mkoa kuwa kitovu cha uchumi kwa mikoa ya magharaibu na nchi jirani za Burundi na DRC.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinna Mathamani ameishukuru Serikali kwa uwekezaji wa miundombinu ya kisasa mkoani Kigoma ambayo inachochea fursa za kilimo, biashara na uvuvi na hivyo kukuza uchumi.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoani kigoma Mhandisi Narcis Choma amemhakikishia Naibu waziri Kasekenya kuwa wamejipanga kuhakikisha daraja la Ruchugi na mzunguko wa Uvinza vinakamilishwa kabla ya mwisho wa mwezi Februari.