Joy FM

Walimu watakiwa kufanya kazi kwa kujituma Kasulu

19 January 2026, 13:06

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu, Picha na Joy Fm

Elimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla na taifa lolote linalotamani maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia haliwezi kufanikiwa bila kuwa na mfumo wa elimu imara.

Na Michael Mpunije

Walimu wa shule za msingi Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha wanafunzi wanaondikishwa kuanza darasa la awali na msingi wanapatiwa elimu Bora.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu wakati akizungumza na baadhi ya waalimu wa shule za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu.

Kanali Mwakisu amesema ili kufikia malengo ya Elimu wilayani humo walimu hawana Budi kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kutatua changamoto zilizopo shuleni kwa lengo la kuongeza hali ya ufaulu na kudhibiti suala la Utoro kwa wanafunzi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu

Baadhi ya waalimu wilayani Kasulu wamesema wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na mwongoza wa sera ya Elimu na Utumishi wa Umma ili kuhakikisha wanaimarisha mahusiano chanya na wananchi katika kusimamia na kufikia malengo katika shule zao.