Joy FM

Wakuu wa shule watakiwa kusimamia ufaulu kwa wanafunzi Kasulu

16 January 2026, 11:38

Afisa Elimu msingi halmashauri ya wilaya ya kasulu Bw. Respis uswetu, Picha na Emmanuel Kamangu

Serikali imesema inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari

Wakuu wa shule za msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kusimama kidete kuhakikisha ufaulu kwa wanafunzi unaongezeka.

Hayo yamebainishwa na wataalamu wa idara ya elimu katika Halmashauriya Wilaya ya Kasulu mmoja wao akiwa Afisa Elimu msingi Bw. Respisi Uswetu wakati wa mafunzo maalumu ya uongozi kwa walimu wakuu wapya wa shule za msingi na sekondari ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kusimamia taluma kwa wanafunzi pamoja kuboresha mazingra ya ufundishahi na ujifunzaji.

Kwa upande wao baadhi ya wakuu wa shule ambao wameshiriki mafunzo haya wameahidi kuhakikisha wanakuwa viongozi bora katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema mipango ya maendeleo ya shule na mbinu za utatuzi wa migogoro.

Hata hivyo walimu hao wameongeza kuwa kwa maarifa ambayo wamepata wanahakika wanaenda kusimamia nidhamu ya utumishi kwa alimu wanaowaongoza ili kuhakikisha wanaiuna kiwango cha taluma za wanafunzi.

Sauti ya Mwandishi wet Emmanuel Kamangu