Joy FM
Joy FM
13 January 2026, 11:04

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imeeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa katika kulinda maji ya mto Nyamironge na kuelekeza kutumia eneo kwa umbali wa mita sito kutoka usawa wa mto
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma Kanasli Evance Mallasa ameomba idara ya madini Mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanaotoa leseni kwa wachimbaji wa madini wanafikisha vibali katika ofisi za wilaya mapema ili kuhakikisha wanatoa maelekezo kwa wawekezaji wa uchimbaji wa madini
Kanali Mallas amesema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, alipotembelea machimbo ya dhahabu Nyamwironge kukagua utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya tarehe 10.12.2025 juu ya uchepushaji wa maji ya mto.
Naye Meneja mradi bonde la ziwa Tanganyika Bona Mremi amesema kitendo cha kuchepusha mto bila kibali ni kosa kisheria.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro ameelekeza kuhakikisha shughuli za uchimbaji zifanyike mita 60 kutoka usawa wa mto.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wilayani Kakonko akiwemo Mbunge wa jimbo la Buyungu wamepongeza maelekezo yaliyotolewa na serikali huku wakiendelea kufanya shughuli zao.