Joy FM

Serikali yaimarisha dhana ya polisi jamii kwa kusogeza huduma

6 January 2026, 10:56

Maofisa wa Polisi wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo kuzuia na kutanzua uhalifu, Picha na ukurasa wa Polisi Tanzania

Maofisa wa Polisi kutoka katika mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Kagera wamepatiwa elimu kuhusu dhana ya Polisi Jamii

Na Mwandishi wetu

Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi jamii limeendesha mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi Jamii kutoka ngazi za Mikoa, Vikosi na Wilaya, kwa lengo la kuimarisha Usalama na kuongeza ufanisi katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kushirikiana na wananchi.

Maofisa wa Polisi wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo kuzuia na kutanzua uhalifu, Picha na ukurasa wa Polisi Tanzania

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Januari 05, 2026 Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, amesema kuwa dhana ya Polisi Jamii ni nyenzo muhimu katika kujenga uhusiano wa karibu kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, hatua inayosaidia kubaini chanzo cha uhalifu na kuzuia vitendo vya kihalifu kabla havijatokea.

CP Shilogile amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuimarisha dhana ya Polisi Jamii kwa kusogeza huduma za Kipolisi karibu zaidi na wananchi na kuwashirikisha kikamilifu katika masuala ya usalama.

Katika mafunzo hayo, washiriki kutoka mikoa mitatu ambayo ni Kigoma, Tabora na Kagera wamepatiwa elimu kuhusu dhana ya Polisi Jamii, Mawasiliano wakati wa Migogoro, Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya Watoto, pamoja na utoaji wa Huduma bora kwa Wananchi.

Maofisa wa Polisi wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo kuzuia na kutanzua uhalifu, Picha na ukurasa wa Polisi Tanzania