Joy FM
Joy FM
26 December 2025, 11:56

Ili kuharakisha maendeleo kwa jamii viongozi hawana budi kushirikiana katika kuwahudmia wananchi na kutatua changamozo azo
Na Hagai Ruyagila
Viongozi wa Serikali na dini nchini wametakiwa kushirikiana kwa karibu na wananchi wao ili kutambua changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati, hatua itakayosaidia kuharakisha maendeleo katika jamii.
Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika, Mhashamu Emmanuel Bwatta, wakati akihubiri katika ibada ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo iliyofanyika Kanisa Kuu la Mt. Andrew Anglikana Kasulu Mjini mkoani Kigoma.

Askofu Bwatta amesema kuwa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi utasaidia kujenga jamii yenye mshikamano, haki na maendeleo endelevu.
Aidha, Askofu Bwatta amewasisitiza waumini wa dini zote nchini kuendelea kudumisha amani, akibainisha kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa na ni urithi muhimu uliowekwa na viongozi wa awamu zilizopita.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Canon Mley, Hosea Nkayamba amewataka wale wote ambao wanavuruga amani iliyopo hapa nchini ni vizuri wakaacha mara moja.

Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Meshack Chunga, amesema utatuzi wa changamoto za kijamii husaidia kuimarisha mshikamano, kudumisha utulivu na kuongeza amani pamoja na kasi ya maendeleo katika jamii.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada hiyo ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo wamesema mahubiri hayo yamewahimiza umoja kudumisha amani maana hakuna maendeleo bila umoja na amani.