Joy FM

Wakristo watakiwa kusherekea krismas kwa upendo Kigoma

25 December 2025, 11:36

Ibaada ya Mkesha wa krismas iliyofanyika katika kanisa la KKKT, Dayosisi ya Magharibi Mjini Kigoma, Picha na Orida Sayon

Waumini wa dini ya Kikristo duniani kutumia Sikukuu ya Krismasi ya mwaka huu kuchagua matendo ya huruma, huku wakizingatia umoja na mshikamano.

Na Orida Sayon

Wakristo Mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kusherehekea sikukuu ya kristmas kwa mazoea badala yake iwe sehemu ya kutengeneza upendo na kupinga ukatili.

Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Jackson Mushendwa katika ibada ya mkesha wa Kristmas Kitaifa iliyofanyika mjini kigoma katika kanisa la KKKT Kigoma.

Askofu Mushendwa amesema kuzaliwa kwa Yesu kristo ni chanzo cha amani na haki hivyo waumini wanapaswa kuwa wamoja ili kujenga mshikamano wa kanisa na Taifa bila ubaguzi.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Jackson Mushendwa
Ibaada ya Mkesha wa krismas iliyofanyika katika kanisa la KKKT, Dayosisi ya Magharibi Mjini Kigoma, Picha na Orida Sayon

Naye Mwenyekiti wa umoja wa kikiristo CCT Manispaa ya Kigoma Mchungaji Tobias Misigaro amelipongeza jeshi la polisi mkoa wa kigoma kwa kusimamia shughuli za ulinzi na usalama huku akiwataka wakristo kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato halali.

Sauti ya Mwenyekiti wa umoja wa kikiristo CCT Manispaa ya Kigoma Mchungaji Tobias Misigaro

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo wameeleza namna walivyojipanga kusherhekea sikukuu ya krismas kwa amani na usalama.

Sauti ya waumini
Waumini wa KKKT wakiwa kwenye mkesha wa krismas, Picha na Orida Sayon

Siku kuu ya Krismasi ni sikukuu ambayo wakristo wanasherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, sikukuu amabyo huadhimishwa kila mwaka disemba 25 ikiwa ni ishara ya ukombozi kwa waumini wa dini ya Kikristo.