Joy FM
Joy FM
23 December 2025, 08:37

Jukumu la msingi la wazazi na walezi ni kuhakikisha watoto wanalindwa, wanalelewa kwa upendo na wanaishi katika mazingira salama ili waweze kufikia ndoto zao na kuchangia maendeleo ya jamii.
Na Prisca Kizeba
Wazazi na walezi wanapotekeleza wajibu wao ipasavyo, jamii hunufaika kwa kuwa na vijana wenye nidhamu na kuepuka ongezeko la uhalifu na vitendo viovu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kituo cha Compassion Mwasenga Robart Petro wakati wa ugawaji wa zawadi za krismasi kwa watoto na wazazi wenye hali ya chini , nakuwaasa wazazi kuwa makini katika uangalizi wa watoto wao.
Sambamba na hayo, Mkurugenzi amewaomba wazazi kuwatia moyo na kuendeleza vipaji vya watoto na kuacha tabii ya kuwavuja moyo pale mtoto anapoonyesha kipaji chake.
Akitoa ufafanuzi wa zawadi hizo, Mhasibu wa Maleni Josephu na kusema kwa wametoa zawadi zenye dhamani ya shilingi milioni sita laki nane na elfu stina na tisa na mia saba.
Baadhi ya wazazi wametoa shukrani zao na hapa wanaeleza furaha yao baada ya kupokea zawadi hizo.